Katika ibada hiyo ambayo pia ilikua ni ibada ya familia ilishuhudiwa ndoa mbili zikifungwa na baada ya kufungwa washarika wote waliohudhuria ibada hiyo, maharusi pamoja na ndugu , jamaa na marafiki zao walishiriki chakula cha mchana ambacho kiliandaliwa na Usharika huo
Ibada hiyo iliongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi huku mahubiri yakitolewa na mchungaji Ernest Kadiva toka ofisi kuu ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani
Pichani juu kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza ikihudumu kwenye ibada hiyo
Maharusi wakipata baraka toka kwa mchungaji Kadiva
Maharusi wakiwa kwenye ibada ya ndoa
Maharusi wakila kiapo kanisani hapo
Baada ya ibada iliandaliwa hafla ya kukata na shoka kanisani hapo ambapo washarika wote , ndugu jamaa na marafiki wa maharusi walihudhuria
Pichani juu ni maharusi wakiwa kwenye hafla hiyo
Mc akiwapa mkono maharusi kwenye hafla hiyo
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Kaanasia Msangi akiwa na mumewe mzee Msangi kulia.Katikati ni mke wa Mchungaji Kadiva( anayesoma gazeti) pembeni kushoto ni mfanyakazi toka Dayosisi ambaye jina lake halikufahamika mara moja
Wageni wakipata vinywaji kwenye sherehe hiyo ambayo ilifanyika kanisani hapo
Ulifika wakati wa kufungua shampaigne, hakika ilikua ni furaha ilioje
Maharusi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wapambe wao
Picha ya pamoja kati ya maharusi na waimbaji wa kwaya kuu ya Usharika wa MwengeMaharusi ni waimbaji wa kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Mwenge
Picha ya pamoja ya maharusi na viongozi wa Usharika wa Mwenge pia viongozi wa dayosisi waliokuwepo kwenye hafla hiyo.Hakika ilipendeza
No comments: