Ibada ya kwanza ilikua ya wanafamilia wote wakati ibada ya pili ilikua ni maalum kwa watu walio kwenye ndoa.Ibada ya tatu ilikua ya wajane na wagane wakati ibada ya nne ilikua ya vijana peke yao
Ibada hiyo iliyoongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi na neno lilifundishwa na mchungaki Enock Kagya
Baada ya mahubiri wanandoa walipata nafasi ya kulishana keki kwa wale waliokuja na wenzi wao na wale ambao hawakuja na wenzi wao walilishwa keki na wachungaji waliokuwepo madhabahuni
Hakika ilikua ni siku nzuri kwani wanandoa wengine wana miaka zaidi ya thelathini na walikumbushana siku yao walipofunga ndoa
Pichani juu mchungaji Kaanasia Msangi akibariki keki hizo tayari ziweze kuliwa
Bwana na Bi Kileo wakikata kata keki tayari kuliwa na wanandoa waliohudhuria ibada hiyo
Bwana Kileo akimlisha mkewe Beatrice ikiwa wakiwa ni wanandoa wa kwanza kufungua zoezi hilo la kulishana keki
Hawa ndio walionunua hizo keki tatu na kuzitoa ziliwe na wanandoa wote waliohudhuria ibada hiyo
Kutoka kushoto ni Bwana na Bi Chonjo, Bwana na Bi Kileo,Bwana Mushi Benn Bwana na Bi Severe na bwana na Bi Uronu
Mzee Uronu akimlisha mkewe keki
Mzee Beny Mushi akilishwa keki na mchungaji
Mzee Severe akilishana keki na mkewe.Hakika iilikua siku ya furaha kwa wanandoa hawa
Mzee Chonjo akimlisha keki mkewe
Bwana Isaya akilishana keki na mkewe
Mzee Rogathe Mushi wakilishana keki na mkewe
Wanandoa wakiwa wamejiandaa kwenda kulishana keki
Baada ya ibada wanandoa walipata nafasi ya kupata picha ya pamoja kama inavyoonekana juu na chini
No comments: