Latest News


More

LISHE ASILI NI DAWA YA WAGONJWA WA MOYO

Posted by : Unknown on : Wednesday, April 30, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :
 
Kula vyakula asili inazidisha miaka ya wagonjwa wa moyo

Wanasayansi nchini Marekani wanasema watu waliowahi kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi maisha marefu iwapo watakula zaidi vyakula ambavyo havijapitia viwandani.

Watafiti walichunguza zaidi ya watu elfu nne waliowahi kupata mshituko wa moyo na kubaini kuwa wana uwezekano mkubwa wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula vyakula hivyo .

Vyakula ambayo havijapitia viwandani vina nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa husaidia katika kuwezesha binadamu kwenda haja bila matatizo.

Vyakula ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.

Hatahivyo wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.

No comments:

Leave a Reply