by : Unknown
Wakina mama wa kanisa waliandaa keki maalum kwa ajili ya mwalimu Lilian Ndegi
Mgeni rasm bwana Paul Makonda kushoto akiwa na mtume Apostle Ndegi (mkuu wa kanisa la Living Water Center - Kawe) na mwalimu Lilian Ndegi ambaye ndiye mwandishi wa vitabu hivyo
Wakina mama wa Kawe wakiunga mkono katika uzinduzi huo wa jumapili
Badhi ya vitabu mbalimbali (pichani juu na chini) ambavyo vimetungwa na mwalimu Lilian Ndegi
Mwalimu Lilian Ndegi akimlisha mgeni rasmi bwana Paul Makonda keki
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Paul Makonda jumapili hii alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitabu vya injili vya mwalimu Lilian Ndegi katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe
Bwana Makonda (pichani juu) alimshukuru mwalimu Lilian Ndegi jinsi Mungu anavyomtumia kuponya roho za watu kwa njia ya vitabu na alisema yuko tayari kushirikiana naye kuhakikisha vitabu hivyo vinawafikia watu wengi zaidi
Pichani juu Bwana Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi wav itabu hivyo
Bwana Makonda akimshukuru Tumaini Kichila kwa ununuzi wavitabu vya mwalimu Lilian Ndegi
Wakina mama wa Kawe wakiunga mkono katika uzinduzi huo wa jumapili
Badhi ya vitabu mbalimbali (pichani juu na chini) ambavyo vimetungwa na mwalimu Lilian Ndegi
Wamama wa Kanisa la Living Water Center Waliandaa keki maalum kwa Mwalimu Lilian Ndegi
Mwalimu Lilian Ndegi akimlisha mumewe Apostle Ndegi KekiMwalimu Lilian Ndegi akimlisha mgeni rasmi bwana Paul Makonda keki
by : Unknown
Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba agano la kale lilipatiwa taifa la Israeli wala sio wakristo. Baadhi ya sheria hizo zilikuwa za kuwafanya waisraeli wajue jinsi ya kumtii na kumfurahisha Mungu (amri kumi za Mungu kwa mfano), baadhi yazo zilikuwa zikiwafunza jinsi ya kumuabudu Mungu (kwa ile njia ya sadaka), nyengine zilikuwa za kuwafanya waisraeli wawe watu maalum (kama sheria za aina za mavazi na chakula). Hakuna sheria yoyote ya agano la kale inayotumika kwetu sasa. Yesu alipokufa msalabani, alimaliza matumizi ya sheria ya agano la kale (Warumi 10:4; Wagalatia 3:23-25; Waefeso 2:15).
Mahali pa sheria ya agano la kale, tuko chini ya sheria ya kristo (Wagalatia 6:2) ambayo ni, “Mpende bwana Mungu wako na moyo wako wote akili zako zote na nguvu zako zote. Hii ndiyo ya kwanza na amri iliyo kuu. na ya pili ni kama ya kwanza, mpende jirani yako kama nafsi yako. Torati yote na manabii inakamilishwa katika amri hizi mbili” (Mathayo 22:37 – 40). Tukifanya mambo haya mawili tutakuwa tunatimiza yale kristo angetaka tuyafanye, “na huu ndio upendo wa Mungu: kutii amri zake. Na amri zake si nzito” (waraka wa kwanza wa Yohana 5:3). Kwa mtazamo, amri kumi za Mungu hazina uhusiano na wakristo. Hata hivyo, tisa katika amri kumi za Mungu zimerudiwa katika agano jipya (zote isipokuwa ile ya kuweka sabato). Kwa kwaida kama tunampenda Mungu hatutakuwa na miungu miginemila yeye. Tukiwapenda majirani zetu hatutawaua, hatutawadanganya,hatutazini nao, wala kutamani kile walichonacho. Kwa hivyo hatuko chini ya sheria ya agano la kale. Sisi ni wakumpenda Mungu na pia majirani zetu. Tukifanya mambo haya mawili kwa uaminifu wa moyo, kila kitu kitakuwa sawa.
Mahali pa sheria ya agano la kale, tuko chini ya sheria ya kristo (Wagalatia 6:2) ambayo ni, “Mpende bwana Mungu wako na moyo wako wote akili zako zote na nguvu zako zote. Hii ndiyo ya kwanza na amri iliyo kuu. na ya pili ni kama ya kwanza, mpende jirani yako kama nafsi yako. Torati yote na manabii inakamilishwa katika amri hizi mbili” (Mathayo 22:37 – 40). Tukifanya mambo haya mawili tutakuwa tunatimiza yale kristo angetaka tuyafanye, “na huu ndio upendo wa Mungu: kutii amri zake. Na amri zake si nzito” (waraka wa kwanza wa Yohana 5:3). Kwa mtazamo, amri kumi za Mungu hazina uhusiano na wakristo. Hata hivyo, tisa katika amri kumi za Mungu zimerudiwa katika agano jipya (zote isipokuwa ile ya kuweka sabato). Kwa kwaida kama tunampenda Mungu hatutakuwa na miungu miginemila yeye. Tukiwapenda majirani zetu hatutawaua, hatutawadanganya,hatutazini nao, wala kutamani kile walichonacho. Kwa hivyo hatuko chini ya sheria ya agano la kale. Sisi ni wakumpenda Mungu na pia majirani zetu. Tukifanya mambo haya mawili kwa uaminifu wa moyo, kila kitu kitakuwa sawa.
by : Unknown
Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung’ang’ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi imesisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.
Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).
Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa. Ni watoe sawa na uwezo wao “ kulengana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi, na mara nyingine kichache kuliko fungu la kumi. Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).
Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).
Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa. Ni watoe sawa na uwezo wao “ kulengana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi, na mara nyingine kichache kuliko fungu la kumi. Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).
by : Unknown
Jibu la Biblia
Mapenzi
ya Mungu ni kwamba umjue Yeye vizuri, umkaribie, na kisha umpende na kumtumikia
kwa moyo wako wote. (Mathayo 22:37, 38; Yakobo 4:8) Unaweza kujifunza jinsi ya
kufanya mapenzi ya Mungu kwa kuchunguza maisha na mafundisho ya Yesu. (Yohana 7:16, 17) Yesu
hakuongea tu kuhusu mapenzi ya Mungu—aliishi kupatana na mapenzi hayo. Kwa
kweli, Yesu alisema kwamba kusudi kuu maishani mwake ni ‘
kufanya, si mapenzi yake, bali mapenzi ya aliyemtuma.’—Yohana 6:38.
Je, ninahitaji ishara, maono, au mwito wa pekee ili nijue Mungu aliniumba kwa kusudi gani?
Hapana,
kwa sababu Biblia ina ujumbe wa Mungu kwa wanadamu. Ina kila kitu unachohitaji
ili ‘
uwe na vifaa kamili kwa ajili ya kila kazi njema.’ (2 Timotheo 3:16, 17) Mungu anataka utumie Biblia pamoja na ‘
nguvu zako za kufikiri’ ili ujifunze mapenzi yake.—Waroma 12:1, 2; Waefeso 5:17.
Je, kweli ninaweza kufanya mapenzi ya Mungu?
Ndiyo,
unaweza, kwa kuwa Biblia inasema hivi: “
Amri za Mungu si ngumu sana kwetu.” (1 Yohana 5:3, Easy-to-Read Version) Hilo halimaanishi kwamba ni rahisi kufuata amri za Mungu kila siku. Lakini, faida unazopata ni nyingi sana zinapolinganishwa na jitihada zako. Yesu mwenyewe alisema hivi: “
Wenye furaha ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika!”—Luka 11:28.
by : Unknown
Jibu la Biblia
Biblia
inataja kuhusu kuchanja chale mara moja tu katika kitabu cha Mambo ya Walawi 19:28, ambapo
tunasoma hivi: “Msijitie alama ya chanjo.” Mungu aliwapa Waisraeli amri hiyo, na
hivyo kuwafanya tofauti na watu waliowazunguka ambao walijitia alama za majina
au maumbo ya miungu yao mwilini. (Kumbukumbu la Torati 14:2) Ingawa Sheria
ambayo Mungu aliwapa Waisraeli haiwahusu Wakristo, tunapaswa kuzingatia kanuni
inayotegemea sheria hiyo.
Je, Mkristo anapaswa kuchanja chale au kuuchora mwili wake?
Maandiko
yafuatayo yanaweza kukusaidia ujue jinsi ya kutenda:
-
“Wajipambe kwa mavazi yenye . . . kiasi.”—1 Timotheo 2:9 New World Translation) Kanuni hiyo inawahusu wanaume na wanawake. Tunapaswa kuheshimu hisia za wengine na kuepuka kujifikiria wenyewe.
-
Wengine wanataka watambuliwe na watu au waonekane wako huru, ilhali wengine wanajichanja chale ili waonyeshe kwamba wanajiamini. Hata hivyo, Biblia inawatia moyo Wakristo ‘watoe miili yao kuwa dhabihu iliyo hai, takatifu, yenye kukubalika kwa Mungu, utumishi mtakatifu pamoja na nguvu zao za kufikiri.’ (Waroma 12:1) Tumia ‘nguvu zako za kufikiri’ kuamua ni kwa nini unataka kujichanja chale. Ikiwa unafanya hivyo kwa sababu unataka kufuata mtindo fulani au kuonyesha kwamba wewe ni mshiriki wa kikundi fulani, kumbuka kwamba kujichanja chale kuna madhara ya kudumu. Kuchunguza nia yako kunaweza kukusaidia kufanya uamuzi wa hekima.—Methali 4:7.
-
“Mipango ya mwenye bidii bila shaka huleta faida, lakini kila mtu anayetenda haraka-haraka bila shaka huuelekea uhitaji.” (Methali 21:5) Mara nyingi uamuzi wa kujichanja chale hufanywa bila kufikiria kwa uzito, na unaweza kuathiri uhusiano wako na wengine au kazi. Ni ghali sana kuchanja chale na kuna maumivu mengi sana unapoamua kuziondoa. Utafiti—kutia ndani biashara iliyositawi ya kuondoa watu chale—inaonyesha kwamba idadi kubwa ya watu waliojichanja chale wanajuta ni kwa nini walifanya hivyo.
by : Unknown
Jibu La Biblia
Katika
Biblia, mara nyingi namba hutumiwa kwa kihalisi, hata hivyo nyakati nyingine
hutumiwa kwa njia ya mfano. Muktadha wa andiko unaweza kutusaidia kujua ikiwa
namba fulani inatumiwa kwa njia ya mfano au la. Fikiria baadhi ya namba ambazo
zinatumiwa kwa njia ya mfano katika Biblia:
-
1 Umoja au muungano. Kwa mfano, Yesu alimwomba Mungu kwamba wafuasi wake “wote wapate kuwa kitu kimoja, kama vile ambavyo wewe, Baba, umo katika muungano pamoja na mimi na mimi nimo katika muungano pamoja na wewe.”
—Yohana 17:21; Mathayo 19:6. -
2 Katika mambo ya kisheria, mashahidi wawili huthibitisha ukweli wa jambo fulani. (Kumbukumbu la Torati 17:6) Vivyo hivyo, kurudia maono au maneno fulani kulihakikisha kwamba jambo hilo lilikuwa hakika na la kweli. Kwa mfano, Yosefu alipokuwa akifasiri ndoto ya Farao wa Misri, alisema hivi: “Kwa kuwa ndoto hiyo ilirudiwa mara mbili kwa Farao inamaanisha kwamba jambo hilo limewekwa imara na Mungu wa kweli.” (Mwanzo 41:32) Katika unabii, “pembe mbili” zinaweza kuwakilisha serikali pacha, kama vile nabii Danieli alivyoambiwa kuhusu Milki ya Umedi na Uajemi.
—Danieli 8: 20, 21; Ufunuo 13:11. -
3 Sawa na vile mashahidi watatu wanavyoweza kuhakikisha kabisa jambo fulani kuwa la kweli, kurudia jambo mara tatu kunakazia au kuonyesha kwamba linalosemwa ni hakika.
—Ezekieli 21:27; Matendo 10: 9- 16; Ufunuo 4:8; 8: 13. -
4 Namba hii inaweza kumaanisha ukamili katika umbo au katika utendaji, kama vile katika maneno “pembe nne za dunia.”
—Ufunuo 7:1; Isaya 11:12; Ufunuo 21:16. -
6 Kwa kuwa namba hii imepungua saba inayowakilisha ukamilifu, sita inasimamia kutokamilika au lisilo kamilifu, au jambo linalohusianishwa na maadui wa Mungu.
—1 Mambo ya Nyakati 20:6; Danieli 3:1; Ufunuo 13:18. -
7 Namba hii hutumiwa mara nyingi kumaanisha ukamilifu. Kwa mfano, Waisraeli waliagizwa na Mungu kuzunguka jiji la Yeriko kwa siku saba, na kuizunguka mara saba katika siku ya mwisho. (Yoshua 6:
15) Biblia ina mifano mingi ambapo namba saba imetumiwa kwa njia hiyohiyo. (Mambo ya Walawi 4:6; 25:8; 26:18; Zaburi 119:164; Ufunuo 1: 20; 13:1; 17:10) Yesu alipomwambia Petro kwamba amsamehe ndugu yake “si, Mpaka mara 7, bali, Mpaka mara 77,” kurudia namba 7 kulionyesha kwamba alipaswa kuendelea kusamehe “bila kuacha”. —Mathayo 18:21, 22. -
10 Namba hii inaweza kuwakilisha jumla ya kitu, au kukusanya pamoja.
—Kutoka 34:28; Luka 19:13; Ufunuo 2: 10. -
12 Namba hii inaweza kumaanisha ukamili kuhusiana na kusudi la Mungu. Kwa mfano, mtume Yohana alipewa maono ya kimbingu ambapo aliona jiji lililokuwa na “mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya hayo majina kumi na mawili ya mitume.” (Ufunuo 21:14; Mwanzo 49:28) Namba 12 ikizidishwa mara kadhaa pia inaweza kuwa na maana hiyohiyo.
—Ufunuo 4:4; 7: 4-8.
Ubashiri kwa kutumia namba
Jinsi
ambavyo namba imetumiwa kwa njia ya mfano katika Biblia ni tofauti na jinsi
inavyotumiwa katika kubashiri. Watu wengine hufanya uchawi kwa kutumia namba,
kupatanisha namba, na kujumlisha namba mbalimbali ili kubashiri matukio. Kwa
mfano, kikundi fulani cha Wayahudi kimechunguza maana zilizofichika kwenye
Maandiko ya Kiebrania kwa kutumia njia inayoitwa gematria, ambayo
inahusisha kutafuta namba fulani ya siri katika namba zinazolingana kwenye
herufi. Ubashiri wa kutumia namba ni namna ya uaguzi, tendo ambalo Mungu
anakataza. —Kumbukumbu la Torati
18:10- 12.
by : Unknown
Ndiyo, hata ingawa Biblia si kitabu cha
kisayansi, inazungumzia mambo ya kisayansi kwa usahihi. Fikiria mifano fulani
inayoonyesha kwamba sayansi inapatana na Biblia na kwamba Biblia yenyewe inataja
mambo hakika ya kisayansi yanayotofautiana na yale ambayo watu walioishi zamani
waliamini.
-
Ulimwengu ulikuwa na mwanzo. (Mwanzo 1:1) Tofauti na hilo, hekaya nyingi za kale zinasema kwamba ulimwengu haukuumbwa, ulijitokeza wenyewe. Wababiloni waliamini kwamba miungu iliyozaa ulimwengu ilitoka katika bahari mbili. Hekaya nyingine zinasema kwamba ulimwengu ulitoka katika yai kubwa sana.
-
Ulimwengu unaongozwa na sheria za asili, si utendaji wa miungu. (Ayubu 38:33; Yeremia 33:25) Hekaya mbalimbali ulimwenguni pote zinafundisha kwamba wanadamu hawawezi kufanya jambo lolote isipokuwa kile kilichoamuliwa na miungu inayotenda mambo yasiyotarajiwa na yenye ukatili.
-
Dunia inaelea angani. (Ayubu 26:7) Watu wengi walioishi nyakati za kale waliamini kwamba dunia ni tambarare na kwamba imeshikiliwa na jitu fulani au mnyama, kama vile nyati au kasa.
-
Maji yanayoingia katika mito na vijito huwa yamevukizwa kutoka baharini au kutoka katika vyanzo vingine kisha yanamwagika tena yakiwa mvua, theluji, au mvua ya mawe. (Ayubu 36:27, 28; Mhubiri 1:7; Isaya 55:10; Amosi 9:6) Wagiriki wa kale walifikiri kwamba maji ya mito yalitoka kwenye bahari iliyo chini ya ardhi, na wazo hilo liliendelezwa hadi karne ya 18.
-
Milima huibuka na kuporomoka, na wakati fulani milima iliyopo leo ilikuwa chini ya bahari. (Zaburi 104:
6, 8) Tofauti na maoni hayo, hekaya fulani zinasema kwamba milima iko jinsi ilivyo leo kwa sababu iliumbwa na miungu. -
Mazoea mazuri ya kutunza usafi hulinda afya. Sheria ambayo Waisraeli walipewa, ilitia ndani maagizo ya kwamba mtu anapaswa kuoga baada ya kugusa maiti, watu waliokuwa na magonjwa ya kuambukiza walipaswa kutengwa, na kinyesi kilipaswa kuzikwa. (Mambo ya Walawi 11:28; 13:
1-5; Kumbukumbu la Torati 23:13) Tofauti na hilo, wakati ambapo sheria hizo zilikuwa zikitolewa, Wamisri walikuwa wakitumia mchanganyiko uliokuwa na kinyesi cha mwanadamu ili kutibu majeraha.
Je, kuna makosa ya kisayansi katika Biblia?
Mtu anayechunguza Biblia kwa akili
iliyofunguka atajibu hapana. Yafuatayo ni maoni fulani yaliyo na kasoro ambayo
watu hutoa kuonyesha Biblia si sahihi kisayansi:
Uwongo: Biblia inasema kwamba
ulimwengu uliumbwa katika siku sita zenye urefu wa saa 24.
Ukweli: Biblia haitoi tarehe
hususa ambayo Mungu aliumba ulimwengu. (Mwanzo 1:1) Pia, siku za uumbaji
zinazofafanuliwa katika Mwanzo sura ya 1 ni
kipindi cha wakati chenye urefu usiojulikana. Kwa kweli, kipindi chote cha
wakati ambacho mbingu na dunia ziliumbwa kinaitwa “siku.” —Mwanzo 2:4.
Uwongo: Biblia inasema kwamba
mimea iliumbwa kabla ya jua ambalo husababisha mfumo wa usanidi-mwanga. —Mwanzo 1: 11, 16.
Ukweli: Biblia inaonyesha
kwamba jua, mojawapo ya nyota zilizo katika “mbingu,” liliumbwa kabla ya mimea.
(Mwanzo 1:1) Katika “siku” ya kwanza ya
uumbaji, nuru ya jua ilipenya angani na kuanza kuonekana duniani. Anga
lilipoendelea kuruhusu mwangaza huo uonekane waziwazi duniani, mfumo wa
usanidi-mwanga ulianza kutenda kazi kwenye mimea katika “siku” ya tatu ya
uumbaji. (Mwanzo 1: 3-5, 12, 13) Baadaye ndipo
jua lilipoonekana waziwazi kutoka duniani. —Mwanzo 1: 16.
Uwongo: Biblia inasema kwamba
jua huzunguka dunia.
Ukweli: Andiko la Mhubiri 1:5 linasema: “Jua limechomoza,
na kushuka, nalo linajitahidi kwa nguvu kwenda mahali pake ambapo litachomoza
tena.” Maneno hayo yanategemea maoni ya mtu anayetazama jua kutoka duniani. Ni
kama vile tu leo tunasema “jua limechomoza” na “jua limetua” hata ingawa ukweli
wa mambo ni kwamba dunia ndiyo inayolizunguka jua.
Uwongo: Biblia inasema kwamba
dunia ni tambarare.
Ukweli: Biblia inapozungumza
kuhusu “miisho ya dunia” inamaanisha “sehemu ya mbali zaidi ya dunia”; maneno
hayo hayamaanishi kwamba dunia ni tambarare wala ina mwisho. (Luka 11:31) Vivyo hivyo, maneno “miisho
minne ya dunia” ni usemi wa mfano unaorejelea eneo lote la dunia na si kwamba
dunia ina pembe nne. —Isaya 11:12; Luka 13:29.
Uwongo: Biblia inasema kwamba
mzingo wa mviringo au duara ni mara tatu ya kipenyo chake, lakini hesabu sahihi
ni pai (π), au 3.1416 hivi.
Ukweli: Vipimo vinavyotajwa
katika 1 Wafalme 7: 23 na 2 Mambo ya Nyakati 4:2 vinaonyesha
kwamba “Bahari ya kuyeyushwa” ilikuwa na kipenyo cha mikono 10 na kwamba “kamba
ya urefu wa mikono 30 ingeweza kuizunguka pande zote.” Huenda vipimo hivyo
vilikuwa tu vya kukadiria. Huenda pia mzingo ulipimwa kwa kutegemea sehemu ya
nje ya bahari hiyo huku kipenyo kikitegemea upande wake wa
ndani.





