Latest News


More

TAG HAMUGEMBE PRAISE AND WORSHIP TEAM KUWEKA WAKFU ALBUM YAO JUMAPILI HII

Posted by : Unknown on : Thursday, August 15, 2013 0 comments
Unknown


Kikundi cha T.AG HAMUGEMBE (pichani juu) cha Bukoba mjini Bwana amewawezesha kutoa album yao mpya ya nyimbo za kumsifu na kumwabudu Mungu.

Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kikundi hiki na mkurugenzi wa vijana wa kanisa hilo ndugu John Mmasi alisema Mungu amewawezesha kurekodi album mpya yenye jina “WEWE NDIWE MUNGU”.

Ndugu Mmasi anasema album hiyo yenye mafundisho mazuri ya Mungu na upako wa kipekee bado hawajaanza kusambaza album yao hiyo na wako kwenye mchakato wa kuanza kuisambaza.


Ndugu Mmasi anasema “watu wajiandae kupokea album hii kwani ina upako wa kipekee” na punde tu wasikiapo album hiyo kwa jina hilo wawaunge mkono kwa kuinunua ili injili ya bwana iendelee kusonga mbele




Ndugu Mmasi anasema watakua na ibada maalum ya kusifu na kuabudu siku ya tarehe 29/09/2013 , ibada ambayo itaanza saa nne kamili asubuhi mpaka saa nane mchana.Mahali ni kanisa la TAG HAMUGEMBE , Bukoba Mjini

Lengo kuu ni kuweka wakfu CD hiyo yenye nyimbo za kusifu na kuabudu iliyobeba jina "WEWE NDIWE MUNGU"

Tarehe 03 Novemba 2013 watafanya tamasha kubwa la uzinduzi wa album hiyo katika kiwanja cha mpira Kaitaba mjini Bukoba kuanzia saa saba mchana

Pesa zitakazopatikana katika uzinduzi huo zitatumika  kwenye kuchangia ujenzi wa kanisa lao kwa maana ya upanuzi, alisema mratibu wa kikundi hichoi bwana Mmasi

“MUNGU AWABARIKI”

Kwa mawasiliano na kikundi hiki wasiliana na mwenyekiti wao ;

John Mmasi - Mwenye kiti wa kikundi na mkurugenzi wa idara ya vijana

Simu ya mkononi: 0752 - 458912

Barua pepe: taghamugembe2013@yahoo.com

No comments:

Leave a Reply